Jeshi la Polisi nchini imetoa ufafanuzi wa taarifa iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii kutoka ubalozi wa Marekani ikionyesha kuwa na uwezekano wa kigaidi nchini na kwamba limeanza kufanyia kazi taarifa hiyo.
Hayo yamebainishwa leo Januari 26, 2023 kupitia taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania makao makuu jijini Dodoma, SACP David A. Misime.
“Jeshi la Polisi limeiona taarifa jana January 25,2023 katika baadhi ya Vyombo vya Habari ikiwepo Mitandao ya Kijamii Kuhusu tahadhari kutoka Ubalozi wa Marekani hapa nchini kwa Wananchi wao kutembelewa na Watu wengi hapa Tanzania wakiwepo Wageni”
“Jeshi la Polisi Tanzania tulianza kulifanyia kazi taarifa hiyo kwa kina toka iliponza kusambaa, hivyo Wananchi wendelee kuwa watulivu na kuendelea na shughuli zao kama kawaida”
“Aidha pale itakapobainika jambo lenye kutia shaka au atakapo onekana mtu/watu wenye kutia mashaka kutokana na mienendo yao, basi taarifa hizo ziripotiwe kwa haraka ili ziweze
kufanyiwa kazi”
“Jeshi la Polisi Tanzania tunapenda kutoa taarifa kuwa, hali ya ulinzi na usalama wa nchi ni shwari kwani matukio makubwa yanayoweza kuleta hofu kwa wananchi yanaendelea kudhibitiwa”