Breaking

Tuesday, 17 January 2023

DKT. DUGANGE AKERWA NA HALI YA UCHELEWESHWAJI WA MIRADI WILAYA YA TARIME



OR TAMISEMI, TARIME

Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Festo J. Dugange (Mb) amewanyooshea kidole halmashauri ya Wilaya Tarime na Halmashauri ya Mji wa Tarime kwa kushindwa kusimamia vizuri fedha za miradi ya maendeleo na kutokamilisha miradi kwa wakati.

Dkt. Dugange ameonesha hali hiyo wakati wa ziara Lake ya kukagua miradi ya Maendeleo katika wilaya ya Tarime ambapo ametembelea na kukagua ujenzi wa kituo cha afya magoma, kituo cha afya nyangoto na Hospitali ya Mji wa Tarime .

Akikagua kituo cha Afya Magoma, amejionea majengo yalioanza kujengwa tangu mwaka 2019 yakiwa yametelekezwa ambayo ni Jengo la Mama na Mtoto, Jengo la maabara, Jengo la Upasuaji na Jengo la mionzi.

Amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri kutumia fedha za mapato ya ndani na fedha kutoka CSR ambayo ni Jumla ya milioni 120 kulingana na Mpango walijiwekea kuhakikisha wanakamilisha majengo yote kabla ya tarehe 1 Machi 2023.

Kadhalika, Katika kituo cha afya Nyangoto amejionea jengo la maabara lilijengwa tangu mwaka 2019 ambalo lipo katika hatua za ukamilishaji lakini limetelekezwa na halijaanza kufanya kazi.

Dkt. Dugange baada ya kujionea Jengo hilo ameagiza halmashauri kufanya tathmini ya ukamilishaji wa jengo la maabara ambalo lipo asilimia 95 ili litengewe fedha na likamilishwe na kuanza kutoa huduma ifikapo tareie 28 Februari 2023.

Vile vile, Dkt. Dugange akiwa katika hospitali ya Mji wa Tarime amejionea ujenzi wa jengo la EMD lililotakiwa kukamilika mwezi wa nane 2022 lakini Mpaka sasa lipo katika hatua ya rangi na uwekaji wa vigae na ameagiza Jengo hilo likamilike ifikapo tarehe 28 Februari 2023.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages