Michael Haight mwenye umri wa miaka 42 nchini Marekani amemuua mke wake, mama mkwe na watoto wake 5 na yeye kujiua baada ya mke wake kuwasilisha ombi la talaka jambo ambalo yeye hakulitaka
Tukio hilo limetokea katika jimbo la Utah nchini Marekani ambapo miili ya watu hao imepatikana ndani ya nyumba ya mashambani katika Jiji la Enoch wakati wa ukaguzi katika boma lao
Waliofariki ni mke wake Tausha mwenye umri wa miaka 40, mama mkwe wake Gail Earl mwenye umri wa miaka 78 na watoto wake watano pamoja na mhusika huyo Michael Haight
Polisi wamesema chanzo cha mauaji hayo ni mwaume huyo kutofurahishwa na ombi la talaka lililowasilishwa na mke wake tarehe Desemba 21/2022.
Via: Eatv