Polisi kaunti ya Uaisn Gishu nchini Kenya wanachunguza mauaji yaliyotekelezwa na watu wasiojulikana baada ya mwili wa mwanaume kupatika kwenye barabara.
Mwili huo ulikuwa umevalishwa nguo za mwanamke na kuwekwa kwenye sanduku na kisha kufunikwa na blanketi.
Wakazi walipatwa na mshangao baada ya kupata sanduku hilo huku uvundo ukiwapiga na ndipo polisi wakaitwa.
Inaarifiwa kuwa sanduku hilo liliangushwa na gari moja ambalo halikuwa na nambari za usajili na kisha likatifua vumbi.
Chanzo: Tuko News