Mwanamume mmoja huko Narok nchini Kenya aliyekwenda kumtafuta mpenzi wake ambaye ni mke wa mtu, ameuwawa baada ya kukutana uso kwa uso na mume wa mwanamke huyo katika kijiji cha Takitech.
Julius Kipkorir mwenye umri wa miaka 42, alikwenda nyumbani kwa mwanamke huyo saa tisa za usiku na alisikika akimuambia afungue mlango ili wale uroda aijue mumewe alikuwepo.
Kulingana na taarifa ya Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Jinai, DCI, mume wa mwanamke huyo aliamka usingizini kwa kushtukia matamshi ya lofa huyo.
Wakati mtu huyo alipobisha mlangi kwa mara nyingine, mume wa mpenzi wake aliibua vita na kumjeruhi vibaya sana.
"Ilichukua juhudi za naibu chifu na wazee wa nyumba kumi kutuliza hali na mambo kurejea kama kawaida," DCI ilisema.
Chero alipoona mambo yamezidi unga, aliamua kutoroka kupitia boma la mifugo, labda kukwepa hamaki za mumewe.
Kipkorir alijeruhiwa vibaya alikimbizwa kupokea matibabu katika Hospitali ya Kapkatet, ila hakufaulu kupona kwani aliaga dunia.
Mume wa nyumba alitiwa mbarini na kwa sasa anazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Abossi, huku akisubiriwa kufunguliwa mashtaka.
Chanzo: Tuko News