Sarah Mwendesha, mwenye umri wa miaka 15 amepandishwa kizimbani leo Januari 5, 2023 katika mahakama ya Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza kwa tuhuma za mauaji.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imeeleza kuwa Sarah nashtakiwa kwa tuhuma za kumuua aliyekuwa mhadhiri katika Kiüvo cha Uhandisi cha Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) Mwanza, Hamida Mussa "Mama Mwakitosi' baada ya kumnyonga kwa kutumia mtandio akiwa nyumbani kwake mtaa wa Buzuruga Mashariki Novemba 26, 2023.
Mshtakiwa huyo ambaye alikuwa msaidizi wa kazi za ndani wa Bi Hamida alikamatwa siku tatu na Jeshi la Polisi baada ya mauaji akiwa wilayani Misungwi alikokimbilia kujificha na alikutwa na mali mbalimbali zilizotambuliwa kuwa ni za Bi Hamida ambaye ni Marehemu.
Mshtakiwa Sarah, amefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilemela, Fortunatus Kubaja kwa ajili ya kesi yake kutajwa kwani mahakama hiyo haina mamlaka ya kisheria kusikiliza kesi hiyo.
Baada ya kufikishwa mahakamani hapo, chini ya ulinzi mkali wa askari Polisi Hakimu, Kubaja ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 19, 2023 itakaposomwa tena.
"Mahakama hii haina mamlaka ya kisheria ya kusikiliza kesi hii ambayo ni ya mauaji hivyo naihairisha hadi Januari 19 Saa 5 asubuhi, Mshtakiwa utaendelea kukaa rumande kwani shtaka linalokukabili halina dhamana," alisema Hakimu Kubaja.