Polisi katika eneo la Navakholo, kaunti ya Kakamega wanachunguza kisa ambapo mwanamume mwenye umri wa miaka 67, anadaiwa kumuua mkewe mwenye umri wa miaka 54.
Marehemu, Rose Atieno alikuwa amemtembelea fundi wa kushona viatu ambaye ni jirani wakati mume wake alipomvamia.
Kwa mujibu wa ripoti ya Citizen, marehemu aligongwa na jembe huku mshukiwa akimtuhumu kwa kutokuwa mwaminifu katika ndoa yao.
Kamanda wa polisi wa kaunti hiyo Joseph Kigen alithbitisha kisa hicho akisema mshukiwa atafikishwa mahakamani punde baada ya uchunguzi utakapokamilika.
Mwili wa marehemu umepelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Kakamega.
Via: Tuko News