Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linamshikilia, Mapinduzi Siliya (45) kwa tuhuma za kumuua mkewe, Terezia Mtajiha.
Siliya anadaiwa kumchinja kwa kutumia kisu kisha mwili kuutupa mto Nzovwe jijini humo.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Benjamin Kuzaga amesema tukio hilo limetokea jana Jumatano Januari 11, 2022 na kwamba mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa kanda ya Mbeya kwa uchunguzi wa kitabibu.
Kuzaga amesema kisa cha mauaji hayo ni mtuhumiwa kumtuhumu mke wake kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine.