Breaking

Sunday, 8 January 2023

AMBAKA DADA YAKE KUPATA UTAJIRI


Frank Kigomba, mwenye umri wa miaka 31, mkaazi wa kijiji cha Kisinga wilaya ya Kilolo mkoani Iringa ameukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na kulipa fidia ya shilingi za Kitanzania Iaki tano kwa kosa la kuzini na maharimu.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imeeleza kuwa hukumu hiyo imetolewa Januari 05, 2023 mbele ya Hakimu wa Mahakama ya wilaya ya kilolo Tumaini Maleko ambapo mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakamani kwa kosa hilo ambapo alisomewa shtaka la kumbaka dada yake wa kuzaliwa Januari 02, 2023 ndani ya nyumba anayojenga kutokana na imani za kishirikina.

Inaelezwa kuwa mtuhumiwa huyo  alidanganywa na mganga kuwa akifanya kitendo hicho atakuwa tajiri.

Baada ya mtuhumiwa kusomewa shtaka lake mahakamani hapo alikirl kosa na hivyo kupewa adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela sambamba na kumlipa dada yake fidia ya kiasi hicho cha fedha.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages