Watu 40 wamefariki na 78 kujeruhiwa katika ajali ya barabarani nchini Senegal.
Rais wa Senegal Macky Sall, ameandika kwenye Twitter kwamba ajali hiyo imetokea katika Kijiji cha Gnivy, mkoa wa Kaffine, saa tisa na nusu usiku.
Rais Sall amesema kwamba amesikitishwa na ajali hiyo na kutuma ujumbe wa kheri kwa familia za waliopoteza wapendwa wao na kuwatakia afueni waliojeruhiwa.
Ametangaza siku tano za maombolezo ya kitaifa kuanzia leo Jumatatu, huku akiahidi kuandaa kikao na mawaziri kujadili namna ya kukabiliana na ajali za barabarani.
Mwendesha mashtaka ya umma Cheikh Dieng amesema kwamba ajali imetokea baada ya gurudumu la basi kupasuka na kupelekea basi hilo kugongana ana kwa ana na basi jingine.
Via: Global Publisher