Watu watano wamefariki dunia papo hapo baada ya lori lililobeba katoni za maji ya kunywa kufeli mfumo wa breki katika eneo la mteremko barabara ya Mwika-Himo na kuigonga kwa nyuma gari dogo la abiria aina ya Toyota Noah lililokuwa likitokea Rombo kwenda Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro.
Ajali hiyo imetokea jioni Jumapili Januari 15, 2023.
Daktari wa hospitali ya Faraja, Samweli Minja amethibitisha kupokea miili ya watu watano na majeruhi wanne.
"Ni kweli tumepokea miili ya watu watano wako mochwari na majeruhi wanne leo hapa hospitalini kwetu," amesema Dk Samweli
Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza anaeleka eneo la tukio na atatoa taarifa baada ya kufika na kuona hali ilivyo
"Naelekea eneo la tukio kulikotokea ajali nikifika nitatoa taarifa kamili,"amesema Kamanda Maigwa
Chanzo - Mwananchi
Chanzo - Mwananchi