Familia ya watu sita akiwemo baba, Khumbulani Togara, mama na watoto wao wanne, akiwemo kichanga, wamefariki dunia katika ajali ya kutisha iliyotokea siku ya Boxing Day, Desemba 26, 2022.
Ajali hiyo iliyozua gumzo kubwa na kuwasikitisha wengi, imetokea nchini Afrika Kusini katika eneo la Musina, wakati familia hiyo ikirejea nyumbani kwao, Zimbabwe baada ya kula Krismasi nchini Afrika Kusini.
Video iliyonaswa na kamera za CCTV, imenasa tukio hilo ambapo familia hiyo ikiwa ndani ya gari aina ya Mitsubishi ‘double cabin’, ilivaana uso kwa uso na lori lililokuwa kwenye spidi kubwa na kusababisha maafa hayo.