Na John Mapepele
Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imepewa cheti cha pongezi kwa kuthamini na kuenzi mchango wa Muasisi na MwenyekQiti wa Kwanza wa UWT hayati Bibi Titi Mohamed.
Pia UWT imempa cheti hicho hicho, kwa Mbunge wa Rufiji na Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe Mohamed Mchengerwa kwa kuthamini na kuenzi mchango wa Muasisi na Mwenyekiti wa Kwanza wa UWT hayati Bibi Titi Mohamed.
Mhe. Chatanda amesema Wizara imepewa Cheti cha Shukrani na UWT Kutambua Mchango wake katika sanaa na kuenzi wapigania Uhuru na maendeleo ya wanawake.
Aidha Mwenyekiti huyo , amesema, Mhe. Mchengerwa amekuwa Kiongozi wa kwanza kuandaa kumbukizi ya Bibi Titi Mohammed iliyofanyika jana na mwaka huu Rufiji, Pwani, kumuenzi Mwanzilishi wa UWT hayati Bibi Titi Mohamed
Aidha amefafanua kwamba kwa kuendesha matamasha mengine, wizara hiyo inachangia katika historia ya kuwaenzi wapigania Uhuru na kuendeleza masuala ya maendeleo hasa ya wanawake.
"Ndiyo maana naipongeza Wizara kwa kuandaa Tamasha kutukumbusha Utamaduni wetu" amesema
Tuzo ya Wizara imepokewa na viongozi wakuu wa Wizara hiyo Waziri Mohammed Mchengerwa, Naibu Waziri Pauline Gekul na Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi.
Aidha amesema, Rais Dkt. Samia ndiyo Bibi Titi Mohamed wa sasa Kwa vile, anaishi maono yake.
Amesisitiza kuwa UWT pia inaamini katika kauli mbiu ya Tamasha inayosem " Mwanamke ni jeshi imara katika kuleta mabadiliko, tumuenzi".