
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya shirika la Posta Tanzania, Brigedia Mstaafu Yohana Ochalla Mabongo. Kufuatia uteuzi huo Waziri wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye amefanya Uteuzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika hilo leo 24/12/22.