Breaking

Friday, 30 December 2022

WATUHUMIWA 1942 WA WIZI WA MIFUGO WAKAMATWA NCHINI


Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi

Jeshi la Polisi kupitia kikosi cha kuzuia na kupambana na wizi wa mifugo nchini limewakamata watuhumiwa 1942 wa wizi wa mifugo kwa kipindi cha Januari hadi Desemba 2022.

Akitoa taarifa hiyo leo Desemba 30,2022 Kamanda wa Polisi Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na wizi wa mifugo hapa nchini kamishina Msaidizi wa Polisi ACP Simon Pasua amesema jumla ya kesi 2934 zimeripotiwa katika vituo mbalimbali hapa Nchini.



ACP Pasua amebainisha kuwa jumla ya mifugo iliyokuwa imeibiwa kwa kipindi cha Januari hadi hadi hivi sasa ni 14530 yenye thamani ya fedha ya kitanzania bilioni 6,719,024,600.


Aidha ameongeza kuwa katika ufuatiliaji jeshi hilo limefanikiwa kukamata watuhumiwa 1942 na kuokoa mifugo 4995 iliyokuwa imeibiwa hapa nchini ambayo thamani yake ni 2,441,127,529.

Vilevile amesema jeshi hilo limefanikiwa kuwafikisha katika mahakamani watuhumiwa wa wizi wa mifugo katika mahakama mbalimbali hapa nchini.

Kamanda Pasua ametoa wito kwa wafugaji na wakulima kufuata matumizi bora ya ardhi ili kuepusha migogoro ya wakulima na wafugaji.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages