Breaking

Wednesday, 7 December 2022

WATU 65 WAKAMATWA TUHUMA ZA WIZI, MADAWA YA KULEVYA, POMBE HARAMU



Jeshi la Polisi Mkoa wa kipolisi Rufiji umekamata watu 65 kwa kujihusisha na tuhuma mbalimbali ikiwemo wizi na madawa ya kulevya. 

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji ACP Protas Mutayoba amesema watuhumiwa hao wamekamatwa kutokana na operesheni ya misako na doria ili kukabiliana na uhalifu na wahalifu wa makosa mbalimbali ndani ya Mkoa huo.

Kamanda Mutayoba amesema kupitia operesheni hiyo jeshi hilo limeweza kukamata wahalifu hao pamoja na vielelezo mbalimbali ikiwemo Madawa ya kulevya jumla ya kilogram 47.765 na watuhumiwa 32, pombe haramu ya moshi lita 118 na watuhumiwa 18, mtambo wa kutengeneza pombe ya moshi mmoja (1) ambao ulitelekezwa huko Mohoro wilaya ya Rufiji.

Amesema operesheni hiyo Imewezesha kupata vielelezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na pikipiki 6 aina tofauti tofauti, zilizokuwa zikitumika katika matukio ya kihalifu.

"Katika operesheni hiyo, Jeshi la Polisi lilifanikiwa kukamata nyara za serikali ambazo ni vichwa viwili Vya mnyama aina ya Nyati pamoja na mtuhumiwa 1"

"Baadhi ya watuhumiwa tuliowakamata katika kipindi hicho wameshafikishwa mahakamani na wengine watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika"
Amefafanua Kamanda Mutayoba

Kamanda ametoa wito kwa wananchi Kuelekea kipindi cha sikukuu za Krismasi, mwisho na mwanzo Wa mwaka, kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili Jeshi la Polisi liwachukulie hatua.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages