NA LUCAS RAPHAEL,TABORA
Walengwa wanaonufaika na mfuko wa maendeleo ya Jamii TASAF katika kata ya Nsololo wilaya y uyui Mkoani Tabora wametakiwa kuacha kutumia fedha wanazopatiwa na serikali kufanya matendo ya anasa badala yake kujiwekea akiba na kuwawezesha kujiinua kiuchumi.
Kauli hiyo jana ilitolewa jana na Diwani wa Kata Nsololo Habibu Sungwa alipokuwa akizungmza na walengwa hao wakati wa uhawilishaji uliofanyika katika kijiji cha Nsololo kata ya Nsololo wilayano humo .
Alisema kwamba fedha wanazozipata wazitumia kwa kujengea uwezo wa kubuni miradi mbaimbali ya maendeleo na sio kutumia fedha hizo kwa anasa jambo ambalo halina tija kwao na familia zao.
Alisema kwamba lengo la serikali kupitia Tasaf ni kujengea uwezo wananchi wake kwa kuondokana na umaskiniwa kipato na kuwafanya kuwa jamii yenye mafanikio makubwa katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo.
Diwani huyo alisema kwamba walengwa wa mfuko huo wanatakiwa kuiga mfano wa Fatuma Habibu ambaye ameweza kuwa na benki ya matofali licha ya hali yake ya kiafya kuwa sio nzuri lakini ameweza kufunga kuku 25 hadi kuwa na Mradi wa tofali za kuchoma 3500 .
Mlengwa wa Tasaf Fatuma Habibu ambaye anasumbuliwa na maumivu makali ya miguu kiasi cha kushindwa kutembea na kusimama kwa muda mrefu alisema kwamba licha ya hali yake hiyo bado anapambana kwa ajili ya kujiinua kiuchumi akishirikia na watoto wake .
Alisema kwamba amekuwa akipata ushirikiano mkubwa kwa mwanaye huyo ambaye amekuwa nguzo ya kuweza kumsaidia katika shughuli mbali mbali alizokuwa anapaswa kufanya mama huyo.
"anashukuru sana kwa kazi kubwa anayoifanya kijana wangu hadi kufikia hapo alipofika sasa ambapo kila kitu mwanaye huyo ndiye anayefanya kutokana na yeye kupata maradhi ya miguu kumuuma kwa kipindi kirefu sasa' anasema Fatuma
Naye mwanae Asia Hamad alisema kwamba toka wajiunge ana mango wa kunusuru kaya masikini wamekuwa na masha mazuri tofauti na kipindi cha nyuma .
Alisema kwamba fedha ambazo wamekuwa wakizipata wamekuwa wajitaidia kuanzisha miradi tofauti Tofauti hadi kufikia kuwa na benki ya matofali ambayo wanauza kwa ajili ya kuongeza kipato .
Alisema kwamba licha ya wao kujiongezea kipato pia wanaajiri watu wengine ka ajili ya kufetua matofali kwani wao pekee yao hawezi ila kwa kushirikiana na jamii wanafanikiwa.
Asia alisema kwamba lengo lao mwaka huu ni kulima mazao mbalimbali ikiwemo Alizeti Eka 4 karanga Eka 2,Viazi ,2 na mihogo 2 wanafanya hivo kutokana na uhitaj wa mvua.
Anaye mratibu wa Tasaf wilaya ya Uyui mkoan hapa Dkt Kija Maige aliwataka walengwa hao kutumia raslimali zilizopo kwenye maeneo yao kwa ajili ya kujiletea maendeleona kujiinua Kiuchumi.
Katika TASAF Awamu ya Tatu Kipindi cha Pili katika wilaya ya Uyui inahudumia zaidi ya vijiji 150, ukiwalenga wale wenye umri kati ya miaka 18 hadi 65 wenye nguvu za kufanya kazi pamoja na wazee wenye umri kuanzia miaka 66 na kuendelea.
mwisho