Breaking

Tuesday, 27 December 2022

WALIOMZIKA MTOTO AKIWA HAI ILI WAPATE MALI WAPANDISHWA KIZIMBANI



Watu watatu akiwemo Zawadi Msagaja (20 mkazi wa kijiji cha Mahaha wilayani Magu mkoani Mwanza, leo Jumanne Disemba 27, 2022 wamepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kumuua mtoto Wake wa kike kwa kumzika akiwa hai ili wapate mali.

Wengine waliofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza na kusomewa shtaka la mauaji ya młoto huyo ni dada yake Zawadi aitwaye Elizabeth Kaswa na mumewe, Mussa Mazuri ambaye ni mganga wa kienyeji.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imeeleza kuwa Akiwasomea shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo, Fortunatus Kubaja, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Mwanahawa Changale aliieleza Mahakama kuwa washtakiwa hao waliłenda kosa hilo Novemba 13 mwaka huu.

Aliendelea kusema, washtakiwa katika kesi hiyo ya mauaji namba 7/2022 waliłenda kosa hilo katika młaa wa Kisundi Kata ya Bugogwa wilayani Ilemela mkoani humo kwa kumzika młoto huyo akiwa hai ili wapate mali kinyume na kifungu namba 196 na 197 cha Sheria ya Kanuni ya adhabu marejeo namba 16 ya mwaka 2022.

"Washtakiwa wołe mchana wa siku hiyo mlishirikiana kumpatia młoto wa Zawadi dawa za kienyeji akalewa kisha mkamfukia akiwa hai na kumsababishia kifo kwa malengo ya kujipatia mali kinyume na sheria," alieleza Changale.

Hała hivyo, washtakiwa baada ya kusomewa shtaka hilo hawakutakiwa kujibu chochołe kwani mahakama hiyo hajna mamlaka kisheria kusikiliza kesi hiyo.

Baada ya washtakiwa kusomewa shtaka linalowakabili, Hakimu Mkazi Mwandamizi, Kubaja aliahirisha kesi hiyo hadi Jumatano Disemba 23, mwaka huu itakapoitwa kwa ajili ya kutajwa.

”Washtakiwa hamtakiwi kujibu chochoÅ‚e kwa sababu mahakama hii haina mamlaka ya kisheria kusikiliza kesi yenu. WoÅ‚e mÅ‚aendelea kukaa rumande kwani shtaka linalowakabili halina dhamana,” alisema Kubaja

Novemba 29 mwaka huu, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kupitia kwa Kamanda wa Polisi Mkoa SACP - Wilbroad Mutafungwa alitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya kukamatwa kwa washtakiwa hao kwa makosa ya kula njama na kumzika młoto wa Zawadi Msagaja (jina linahifadhiwa) kama kafara ili wajipatie utajiri jambo ambalo ni kinyume na sheria na kukiuka haki za binadamu.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages