Breaking

Wednesday, 28 December 2022

WALENGWA TASAF SIKONGE WATAKIWA KULIMA MAZAO YANAYOSTAHIMILI UKAME




Na Lucas Raphael,Tabora

Walengwa wa Tasaf wilayani sikonge mkoani Tabora wameshauriwa kulima mazao yanayo stahimili ukame kulingana na kuwepo kwa mvua kidogo inayoratajia kunyesha msimu huu wa kilimo.

Wito huo umetolewa jana na Afisa Kilimo kata ya Pangale na Mwezeshaji wa walengwa wa Tasaf Josephine Mzoo wakati wa uhawilishaji uliofanyika katika kijiji cha kipanga kata ya kipanga Mlimani wilayani Sikonge mkoani hapo.

Alisema kwamba wakulima wanapaswa kulima mazao kinga njaa ambayo ni Viazi na Mihogo ili kuweza kukabilia na njaa inayoweza kujitokeza katika msimu wa kilimo mwaka huu .

Josephine aliendelea kusema kwamba mvua za mwaka huu ni chache kulingana na utabiria wa hali ya hewa unaonyesha kuwa mvua zitanyesha chini ya wastani.

Naye mlengwa wa Tasaf katika kjiji cha Kipanga mlimani na kata ya Kipanga Nelea Katumbo alisema kwamba watajitaidi kulima mazao yanayostamili ukame ili kuweza kupata chakula katika msimu huu wa kilimo .

Alisema kwamba licha ya kulima mazao hayo pia amefanikiwa kufunga kuku na kisha kuweza kununua mbuzi na sasa ana mbuzi 11 ambao analengo la kuunza a kununua Ng’ombe .

Alisema kwamba toka kujiunga na mfuko huo amefanikiwa kimaisha kwa kuweza kujiudumia kwa chakula ,kuweza kumudu kulima mazao mbalimbali kwa pesa anayopata, anatoa pesa nyingne kwa ajili ya mahitaji ya wanafunzi na chakula inayobaki kwa ajili ya mbole kwa ajili ya shamba .


Alisema kwamba licha ya kutumia mbole ya samadi kwenye mashamba lakini pia anatumia mbole ya madukani kwa ajili ya kupata mazao bora.

Naye Zafarani Hussein alisema kwamba kulingana utabiri wa hali ya hewa unaosema mvua za mwaka huu zitanyesha chini ya wastani jambo ambalo wanalazimika kulima mazao yanayostahimili ukame.

Alisema ushauri huo ulitolewa na afisa kilimo wanauchukuwa kwa jicho la Tatu kutokana na mvua kunyesha kwa kiwango kidogo ila watajitaidi kuyatunza mazao ambayo tayari wameyapanda

Hata hivyo malengo hayo amekiri kunufaika na mpango wa kunusuru kaya masikini – Tasaf kwa kuweza kusomesha watoto, kuanzisha miradi kufunga mbuzi ,kuku, bata na Ngombe.


Alisema kuwa tangu ajiunge na TASAF ambapo kwa mwaka huu ameweza kulima na anatarajia kupata gunia 8 za mahindi, lengo ni kuongeza kulima mazao ya kilimo hasa Karanga, Muhogo na kuongeze idadi ya kutoka mbuzi 10 hadi kununua Ng’ombe wa 3 kwa ajili ya kumsaidia kulima mashamba yake .


Alisema kwamba licha ya kununua Ng’ombe hao pia amenunua jembe la kukokotwa na Ng’ombe kitu ambacho kitamsaidia kulima mashamba makubwa kikubwa kuona mvua inayesha vizuri .

“Tunaishukuru sana serikali kwa kutuondolea umaskini huku vijijini kwetu, kama sio fedha hizo mimi ningekuwa nimeshakufa, lakini kutokana na fedha hizo zimemsaida kimaendeleo”alisema Zafarani Husein

Mratibu wa mfuko wa maendeleo ya Jamii wilaya ya sikonge’ Claud Nkanwa Alisema walengwa wameendelea kupewa mafunzo ya kujiwekeza katika raslimali zalishi ili pindi mpango huo utakapoisha au kipindi chao kitakapoisha waweze kujiwezesha kuendelea na Maisha yaliyo bora .


Hata hivyo aliwataka wananchi wanaonufaika na mpango huo wa kunusuru kaya masikini TASAF kuzitumia fedha hizo kama ambavyo wamekuwa wakifundishwa na viongozi wa TASAF huku akisema yeye atakuwa mfuatiliaji wa fedha hizo.



Mwisho

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages