Breaking

Friday, 23 December 2022

RAIS DKT. SAMIA AMWAGA MAMILIONI KWA WASANII, WAZIRI MCHENGERWA AWATAKA WAJITOKEZE KUKOPESHWA NA MFUKO WA SANAA



Na John Mapepele

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa ametoa hundi za mamilioni ya fedha kwa wadau waliokidhi kukopa kwenye mfuko wa Utamaduni na Sanaa na amewataka wasanii na wadau wa kazi za sanaa kujitokeza kwa wingi kuomba kukopeshwa fedha kutoka kwenye mfuko huo alioufufua Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kuwakwamua kiuchumi.

Mhe. Mchengerwa amesema haya leo Disemba 23, 2022 jijini Dar es Salaam akiwa na Katibu Mkuuwa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi kwenye uzinduzi rasmi wa utoaji mikopo kutoka kwenye mfuko huo ambapo uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na viongozi na wadau mbalimbali wa Sanaa na Utamaduni.




Aidha, wakati wa uzinduzi huo wadau wa tano kati ya kumi na tisa waliowasilisha maombi yao walipatiwa fedha za mfuko huo.Amefafanua kuwa dhamira ya Serikali inayoongozwa na Rais Samiaa ni kuona kuwa kila Mwananchi (msanii au mdau wa sanaa) mwenye sifa ya kukopa kwenye mfuko aweze kupata fedha ya kuboresha kazi zake. 

“Naomba nieleweke vizuri fedha hizi ni za kila mtanzania, kila mwana sanaa, kila Kijiji, kila kata, kila wilaya, kila mkoa, yule ambaye anaamini ana kazi yake ameitengeneza, yule ambaye anaamini ameandaa muswada wake vizuri, awe Tanga awe Dodoma awe songea, awe Mtwara atazipata ikiwa tu ana sifa” amefafanua Waziri Mchengerwa.



Amelielekeza Baraza la Sanaa nchini kuandaa utaratibu wa kutengeneza mfumo ya kimtandao ambao utawafanya waombaji kutoka sehemu mbalimbali nchini kuweza kuomba wakiwa huko huko na kupatiwa huduma badala ya kusumbuka kuja Dar es Salaam.

Awali amewataka watendaji kujiongeza kwa kushirikiana na wadau ili kupata fedha zaidi za kuwasaidia wasanii ili waweze kuwakopesha viwango vikubwa ambavyo vitakidhi matakwa ya waombaji hao.

Katika uzinduzi huo Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hassan Abbasi alimtambulisha Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Utamaduni Sanaa, Bi.Nyakaho Mturi Mahemba
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages