Breaking

Wednesday, 14 December 2022

RAIS DKT. SAMIA AFANYA UTEUZI WA MAKATIBU WAKUU


Na lango la habari

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa makatibu wakuu wawili wa wizara.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo jumatano Disemba 14, 2022 na Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais ikulu Zuhura Yunus imeeleza kuwa Rais Dkt. Samia amemteua Dkt. Hashil Twaib Abdallah kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Abdallah alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara (Uwekezaji).

Aidha Rais Dkt. Samia amemteua BW. Kaspar Kaspar Mmuya kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi.

Kabla ya uteuzi huo BW. Mmuya alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu).

Taarifa hiyo imeeleza kuwa uteuzi huu ni kuanzia tarehe 09 Desemba, 2022.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages