Calista Haule (15) mkazi wa kijiji cha Lifua kata ya Luilo wilayani Ludewa mkoani Njombe amefariki baada ya kupigwa na radi wakati akiwafunga mbuzi chini ya mti baada ya kuwatoa malishoni.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema binti huyo alipigwa na radi hiyo na kufa papo hapo sambamba na mbuzi aliokuwa akiwafunga
Baba wa binti huyo pamoja na dada yake wameelezea masikitiko yao na kudai kuwa binti huyo alirejea nyumbani wiki moja iliyopita akitokea shuleni Mafinga mkoani Iringa kwa ajili ya likizo baada ya shule kufungwa.
Via: EATV