Breaking

Friday, 23 December 2022

NAIBU WAZIRI KATAMBI AONGOZA KIKAO KAZI CHA TATHMINI NA MIKAKATI YA UTEKELEZAJI MAJUKUMU OFISI YA WAZIRI MKUU



Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amekutana na kufanya mazungumzo na Menejimenti ya ofisi hiyo hii leo tarehe 23 Disemba, 2022 katika jengo la OSHA, jijini Dodoma.

Lengo la kikao kazi hicho ni kufanya tathmini na kupanga mikakati ya utekelezaji wa majukumu ya ofisi hiyo.



Akizungumza na menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mheshimiwa Katambi amewataka viongozi hao kuendelea kuchapa kazi kwa bidii, ufanisi, kushirikiana na kuwa wabunifu katika kutekeleza majukumu yao ili kufikia matarajio ya Serikali na wananchi wanaowahudumia.


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages