Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Yusuph Makamba ameizungumzia kauli ya Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, Dkt. Bashiru iliyotafsiriwa kuwa amebeza kitendo cha Rais Dkt. Samia kuambiwa anaupiga mwingi.
Novemba mwaka huu, Dk Bashiru akihutubia mkutano wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (Mviwata) uliofanyika mkoani Morogoro, aliwataka wakulima kudai haki zao, huku akionyesha kukerwa na kauli ya kuupiga mwingi.
“Nina Shemeji yangu pale ana tatizo na kuupiga mwingi na kuna mwingine alisema hapa kuupiga mwingi ni kiswahili cha Mjini, sio kiswahli cha Mjini ni nahau, kuupiga mwingi maana yake ni Mtu aliyefanya kazi nyingi na kubwa”
“Mimi ndio Mwenyekiti wa Makatibu Wakuu Wasaidizi Mimi Mwenyekiti wao walinichagua jana, tulimwambia Dr.Bashiru, Magufuli Dr. Bashiru akasema ni Bulldozer wewe akakuita Jembe, wenzako sasa wameamua kutomuita Jembe wamesema anaupiga mwingi tatizo nini?, ajenda hiyo imeisha sasa"
Aidha Mzee Makamba amesema katika Nchi hii wanaoupiga mwingi ni Watu wawili tu Rais Dkt. Samia na Rais Dkt. Mwinyi huku akisema haoni kama ni sahihi kusema Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya au Viongozi wengine kuwa nao wanaupiga mwingi.“Nimemsikia Mjumbe mmoja hapa kutoka Pemba Kusini anasema Mkuu wa Mkoa ameupiga mwingi kama Dr.Hussein Mwinyi, haiwezekani wanaopiga mwingi ni wawili tu Rais wa Jamhuri ya Muungano (Dkt.Samia Suluhu) na Rais wa Zanzibar (Dr.Mwinyi) Mkuu wa Mkoa anaupiga mwingi, ana hela?”
“Mkuu wa Wilaya anaupiga mwingi ana hela? hata kuahidi kwenye Kijiji, Mkuu wa Wilaya kwamba nitaleta maji hawezi anakuja kwa Rais Samia, sasa nani anaupiga mwingi?, msichanganye mambo, nyie wengine wote ni Majembe wanaoupiga mwingi ni wawili tu katika Nchi hii CCM oyee, “