Mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Masaki mkoani Pwani aitwaye Lasmin Kondo, amefariki dunia kwa kujinyonga mwenyewe kwa kile kilichoelezwa kuwa ni baada ya wazazi wake kumkataza kujihusisha na mapenzi.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoani Pwani ACP Pius Lutumo, amesema katika tukio la kwanza la mwanafunzi kujinyonga lilitokea mnamo Desemba 19, 2022, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni baada ya kugombezwa na wazazi wake kutojihusisha na mambo ya mapenzi kufuatia kukutwa na barua aliyokua amemuandikia mpenzi wake.
Aidha Kamanda Lutumo amelitaja tukio la mwanamke mwingine aliyekuwa ameuawa na mwili wake kuharibika kwa kile kilichotajwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Via:EATV