Breaking

Wednesday, 14 December 2022

MTOTO WA MIAKA TISA ANUSURIKA KULIWA NA MAMBA AKIOGELEA MTONI



Mtoto wa miaka tisa amenusurika kifo kutokana na shambulio la mamba katika wilaya ya Chibuto katika mkoa wa kusini mwa Msumbiji wa Gaza.

Msichana huyo alikuwa akiogelea katika mto Limpopo wakati tukio hilo lilipotokea.

Aliviambia vyombo vya habari nchini humo kwamba alipogundua kuwa alikuwa amekamatwa na mamba huyo , alijaribu kukwaruza pua ya mnayama huyo hatari ,hali iliyosababisha puani na kumtema, ambapo mtoto huyo alipata majeraha mabaya kwenye moja ya miguu yake.

"Mamba alinishika na kuniburuza hivyo nikampiga na kukwaruza pua yake .Kisha mamba huyo aliniachilia mara moja na kunitupa," alisema mtoto huyo.

Mara moja alipelekwa hospitali ya wilaya kwa matibabu. Marta Moiane, mkurugenzi katika hospitali hiyo, amesema msichana huyo yuko katika hali nzuri kiafya.

Dkt Moiane alisema hili ni tukio la pili la shambulizi la mamba katika hospitali hiyo mwaka huu kutokana na shambulio la mamba.

Mashambulizi ya mamba ni ya kawaida katika mito mikubwa ya Msumbiji .
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages