Breaking

Wednesday, 28 December 2022

MTOTO WA MIAKA MITATU ALIWA NA FISI - MWANZA



Mtoto Emanuel Marco Nyagela mwenye umri wa miaka mitatu mkazi wa Kijiji cha Mwangika kata ya Mwabomba wilayani Kwimba mkoani Mwanza amefariki dunia baada ya kuliwa na fisi wakati akienda kuoga kwenye dimbwi akiwa na wenzake.

Tukio hilo jana Desemba 27/2022 saa 12 jioni kijijini hapo baada ya mtoto huyo kunyakuliwa na Fisi na kutokomea nae kuelekea msituni.

Baba wa mtoto huyo aitwaye Marco Nyangela amesema alisikia yowe kutoka kwa wanakijiji wakisema mtoto wake ameliwa na fisi ndipo wakaanza kumsaka mtoto huyo na kuishia kuona damu zikiwa zimetapakaa kuelekea kwenye msitu huo.

Hadi kufikia leo Desemba 28/2022 asubuhi wamefanikiwa kuona nguo alizokuwa amevaa mtoto huyo, fuvu la kichwa, ubongo pamoja na meno mawili.

Germanus Masala ni mwenyekiti wa kijiji hicho na Amede Ssteness àmbae ni diwani wa kata ya Mwabomba wamesema wataendelea kushirikiana na wanakijiji kuwasaka fisi hao huku wakiwataka wazazi kuwa makini na watoto wao hasa nyakati za usiku.


CHANZO - EastAfricaTV
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages