Breaking

Thursday, 22 December 2022

MTOTO WA MIAKA MITANO AKUTWA NA VYUMA 52 TUMBONI




Mtoto mwenye umri wa miaka mitano amenusurika kifo baada ya kumeza vyuma 52 kutoka kwenye kifaa cha kuchezea.

Mvulana huyo alilazimika kupasuliwa tumbo sehemu tano ili kuondoa vyuma vilivyokuwa vimekwama tumboni mwake.

Mama yake mtoto huyo Lyndsey Foley alisema alihofia kuwa mtoto wake angefariki na kutoa tahadhari kwa wazazi wenzake kuwa makini wanapowanunulia wanao vifaa vya kuchezea.

Foley, 34, alisema alianza kuwa na wasiwasi baada ya mtoto wake kushindwa kupona baada ya kuugua kwa wiki kadhaa.

Wakati hali ya mwanawe iliendelea kuzorota, alimpeleka mwanawe Jude katika hospitali ya Prince Charles mnamo Agosti 2022, akiwa na maumivu makali.

Alipomfikisha katika hospitali hiyo, uchunguzi na kipimo cha X-ray vilibaini kuwa alikuwa na vyuma tumboni.

Wizara ya afya ya Wales (PHW) imewatoa wito kwa watu kuwa makini na kufikiria kabla ya kununua bidhaa kwa ajili ya watoto wao zenye vyuma vidogo na betri na vifungo.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages