Breaking

Thursday, 29 December 2022

MWANAFUNZI DARASA LA NNE AJICHIMBIA KABURI NA KUJIUA KISA NGUO ZA KRISMASI



Mvulana mmoja wa miaka 11 amejiua katika kijiji cha Kibongoti, kaunti ya Kirinyaga nchini kenya sababu kuu ikiwa babu na nyanyake kuchelewa kumnunulia nguo mpya za siku kuu ya Krismasi.

Akithibitisha kisa hicho, mkuu wa polisi eneo hilo Moses Koskei alisema kuwa uchunguzi katika kifo cha mwanafunzi huyo wa darasa na nne umeanzishwa na maafisa wake.

Koskei alisema kuwa mamake mwendazake ambaye hufanya kazi nchini Qatar alikuwa ametumia wazazi wake pesa za kumnunulia mjukuu wao nguo mpya.


Hata hivyo nyanya na babu walimtaka mjukuu wao kuwa mvumilivu na kusubiri kupata nguo mpya baada ya Krismasi kwa sababu ya bei ya sasa ya nguo.

“Inakaa alikuwa ameongea na mamake ambaye alimthibitishia kuwa alikuwa ametuma pesa. Ninadhani alichukulia ombi la subira kutoka kwa nyanya na babu yake kama kukataa kumnunulia nguo mpya,” Koskei alisema.

Nyanyake Rose Ritho alisimulia jinsi mtoto huyo huyo alivyokuwa amechimba shimo refu katika boma hilo kabla ya kisa hicho.

Alipomuuliza mtoto huyo alimwambia kuwa alikuwa anapanga kupanda mgomba wa ndizi katika shimo hilo.

Nyanya alimuonya na kumtaka alizibe akimwelekezea kuwa ni hatari kuwa na mgomba wa ndizi karibu na waya wa umeme.

Chanzo: Tuko News
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages