Mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 23 anauguza majeraha mabaya kichwani baada ya kukatwa na mke wake kufuatia mzozo wa nyumbani.
Hazraj Latif Byakika raia wa Uganda anaripotiwa kushambuliwa na mke wake Fauzi Namuli mnamo Ijumaa - Disemba 23 - baada ya kushinda kupata hela za kumpa asuke nywele zake kwa ajili ya sherehe za Krismasi.
Gazeti la New Vision linaripoti kuwa Fauzi alimshambulia mume wake akimtaka vibaya kichwani kwa kutumia panga. Mwanamume huyo alipiga kamsa akiitisha msaada na majirani walipofika, walimkuta akihema na chirizi la damu likitoka kichwani kwake
Latif alikimbizwa katika kituo cha afya cha Kakooge nchini humo kwa huduma ya kwanza kabla ya kupelekwa katika Hospitali ya Kamuli kwa matibabu zaidi.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya hali yake kudhibitiwa, Latif alisema kuwa mke wake aliaza kuagiza pesa za kusuka nywele zake wili mbili zilizopita.
Aliahidi kumpatia pesa hizo kabla ya siku ya Krismasi - Disemba 25 - lakini hilo halikutumia kutokana na ugumu wa kifedha anaopitia kwa sasa.
Kufuatia kisa hicho, Fauzi alitoweka na kwa sasa anasakwa ili kujibu mashtaka ya jaribio la mauaji na kumsababishia mwenzake majeraha ya mwili.