Breaking

Monday, 19 December 2022

MHUBIRI AUAWA KWA KUPIGWA MAWE NA WANACHI WENYE HASIRA




Mhubiri mmoja kutoka nchini Uganda alikumbana na mauti yake mikononi mwa wanakijiji waliokuwa na hasira baada ya kupatikana karibu na eneo la mauaji.


Inaripotiwa kuwa Mchungaji Julius Mugisa alikuwa miongoni mwa genge lililomuua Tobias Komunda nyumbani kwake katika kijiji cha Igogonya mnamo Ijumaa, Desemba 16,2022.


Washukiwa hao walikuwa wamesafiri hadi nyumbani kwa mwathiriwa wakitumia gari ambalo bado nambari lake la usajili haijajulikani.


“Inadaiwa genge la watu watano wasiojulikana waliokuwa wakisafiri na gari jeupe na namba ya usajili ambayo haijajulikana, walikwenda nyumbani kwa marehemu (Komunda) mwendo wa saa kumi na moja jioni. Wote walienda nyuma ya nyumba ya Komunda ambapo walitumia takribani dakika 30."


"Walianza kutofautiana kabla ya Komunda kuwaambia waondoke nyumbani kwake. Yeye (Komunda) alijaribu kuwapiga kwa jiwe lakini alipigwa risasi ya kichwa na kufa,” mtu aliyeshuhudia aliwaambia polisi.


Chanzo cha mzozo huo bado hakijajulikana, kama Daily Monitor inavyoripoti. Baada ya mauaji hayo, washukiwa hao walitoroka katika eneo la tukio wakitumia gari na kumwacha Mugisa.


Jitihada zake za kuhepa kama wenzake ziliambulia patupu baada ya wakazi wa waliokuwa na hasira kumpata na kumvamia.


“Mchungaji alikimbia kutoka eneo la tukio lakini tayari alikuwa ametambuliwa na wakazi waliokuwa wakijibu milio ya risasi.


Alishambuliwa na kupigwa na umati mkubwa wa wakazi wenye hasira ambao waliwazidi nguvu maafisa wa polisi wa eneo hilo waliojaribu kumwokoa,” mtu mwingine aliyeshuhudia alisema.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages