Breaking

Thursday, 15 December 2022

MCHUNGAJI AKUTWA AMEFARIKI AKIFUNGA SIKU 30




Abdel Raphael (42) Mkazi wa Mtaa wa Uwanja halmashauri ya mji Geita amekutwa amefariki ndani kwake akiwa kwenye mfungo wa siku 30 akitarajia kufufuka Desemba 8

Mmoja wa waumini waliokuwa wakishiriki ibada ya pamoja na marehemu ambaye alikuwa mchungaji wao anasema marehemu aliwaaminisha kuwa ifikapo Desemba 8 atafufuka lakini kufikia siku hiyo akawa amefariki na mwili wake kuharibika

"Ameingia ndani amelala kwenda tarehe 3 kumwangalia tukakuta mwenzetu amebadilika sasa tukajiuliza ndio haya aliyoyasema kwamba anabadilishiwa mwili kwenda kufanya huduma, lakini cha ajabu tangu tarehe 2 hiyo alivyofariki usiku tukiwa kwenye maombi anakuja anakushika begani anakushika mkono mtu yeyote akiwa amelala usiku anamwambia amka muendelee kuomba, tukaendelea kuomba tukajua Labda ni kawaida alivyokuwa amedai lakini siku tunaona zinazidi kwenda", alisema John

"Tulikuwa tumefunga tangu tarehe 28 mwezi wa 11 ilivyofika tarehe 2, kwenye chumba chake cha maombi kumcheki alikuwa mzima, tarehe 3 kwenda kumwangalia Ile hali ilitutisha tukakuta ameanguka kitandani yupo kifua wazi yupo kwenye bukta ikabidi tumkusanye miguu tumuoshe vizuri tukamfunika mdomo macho vizuri tukamlaza vizuri alafu tukaenda kutoa taarifa katika uongozi wa mtaa kwa ajili ya taratibu zinazofuata", alisema Zuberi.

Via: EATV
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages