Wakazi wa Lari katika kaunti ya Kiambu nchini Kenya waliwachwa vinywa wazi baada ya mama mmoja na bintiye kuteketea kwa moto ndani ya nyumba yao.
Katika tukio hilo la Jumapili, Disemba 19, lililotokea usiku wa manane, wawili hao waliteketea hadi kufa baada ya nyumba yao ya mbao kushika moto.
Kwa bahati mbaya, majirani ambao waliitikia kilio cha huzuni wa wawili hao walishindwa kuzima moto huo.
Baadaye walipata miili yao ambayo ilikuwa imechomeka na kuwa majivu.
Polisi wameanzisha uchunguzi kuhusu tukio hilo la kusikitisha ambalo linashukiwa kuwa la uchomaji moto.