Breaking

Friday, 16 December 2022

MAMA AUWA WATOTO WAKE WAWILI KISHA AJINYONGA



Amina Maketu mwenye umri wa miaka 34 amewaua watato wake wawili wenye umri wa miaka 9 na mwingine ana umri wa mwaka 1 na miezi 8 na kisha yeye mwenyewe kujinyonga huku chanzo cha tukio hilo ikiwa ni ugomvi wa ardhi uliotokea kwenye familia yake.


Akielezea tukuio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Michael Chilya, amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Desemba 15,2022, katika mtaa wa Namanditi A, Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, huku sababu ya kutokea tukio hilo ikiwa ni ugomvi wa ardhi alikuwa anagombea yeye na ndugu zake ambapo marehemu ameacha ujumbe unaoeleza kuwa ameamua kujiua yeye na kuua watoto wake ili watoto wake wasipate tabu.

Akieleza kwa masikitiko makubwa Peter Komba ambaye ni mume wa marehemu amesema anasikitishwa na kitendo cha mke wake huyo kuwaua watoto wake kwani hakuwa na ugomvi naye licha ya kutengana naye.

Pololety Kamando Mgema mkuu wa wilaya Songea naye alifika mpaka eneo la tukio ambapo amewaomba majirani kutoa ushirikiano kwa polisi wakati wa uchunguzi wa vifo hivyo.


Via: EATV
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages