Breaking

Thursday, 15 December 2022

MAKAMU MWENYEKITI UWT TAIFA ASHIRIKI TAMASHA LA BIBI TITI, WAZIRI MCHENGERWA AOMBA SIKU MAALUM YA WANAWAKE



Na John Mapepele

Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bi. Zainabu Shomari amewasili Ikwiriri-Rufiji kwa ajili ya kushiriki kwenye Tamasha la kumbukizi la Bibi Titi Mohamed.

Tamasha hili limeanza leo Jumatano Disemba 14, 2022 ambapo usiku wa leo kunafanyika dua maalum ya kumwombea hayati Bibi Titi.


Tamasha hili linaloratibiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa Rufiji, Mhe. Mohamed Mchengerwa ambaye pia ni Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo linatarajia kumalizika kesho.

Kwa mujibu wa ratiba kesho, tamasha litaanza Kwa kongamano maalum la kujadili mchango wa Bibi Titi ambapo mada mbalimbali ziliwasilishwa na jioni kupambwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali.



Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Mhe. Abdurahaman Kinana anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi.

Mhe. Mchengerwa ametoa wito kwa wananchi wote kujitokeza kushiriki katika Tamasha hili la kihistoria.


Amesema Bibi Titi alifanya harakati kubwa Sana za kuleta uhuru katika Taifa letu na kuomba kuwa na siku maalum ya mwanamke ikiwa ni njia pekee ya kumuenzi mchango wa mwanamke.

Aidha, amesema Tamasha hili litasaidia kutoa hamasa ya kizazi cha sasa kutambua na kuthamini uzalendo.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages