Watu 57 wamenusurila kifo katika ajali iliyotokea barabara kuu ya Morogoro - Dar es-salaam baada ya gari ya abiria kampuni ya Al-Seady lililokua linatoka Kilosa kuelekea Dar es Salaam kupinduka eneo la Kitungwa Manispaa ya Morogoro.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Fortunatus amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi la Ally's Star lililokua linatokea Dar es salaam kuelekea Mwanza kutaka kuyapita magari yaliyopo mbele yake bila kuchukua tahadhari ndipo dereva wa gari la Al Saedy alimkwepa kuepusha gari kugongana USO Kwa USO ndipo likapinduka hata hivyo dereva aliyesababisha ajali hiyo anashikiliwa na jeshi la polisi.
Kaimu Kamanda wa Jeshi za Zimamoto na Uokoaji Mkoa Morogoro Emanuel Ochieng amesema abiria 17 wamepata majeraha madogo na jeshi la zimamoto na uokoaji limewapatia huduma ya kwanza na kuendelea na safari huku Kondakta wa basi hilo amekimbizwa hospitali ya Rufaa Mkoa Morogoro kupata matibabu zaidi baada ya kupata majeraha makubwa.
Kwa upande wake Mkuu wa kikosi cha usalama Barabarani mkoa wa Morogoro Mrakibu wa Polisi Zauda Mohamed Gari hilo lilipunduka katika harakati za kukwepa Gari linguine Basi la Abiria kampuni ya Ally’s lilitokea Dar es Salaam kwenda Mwanza lililotaka kuyapita magari mengine bila Tahadhari na kutaka kukutana Uso kwa Uso na basi hilo lililopinduka.
Ajali hii imetokea ikiwa imepita siku tatu tangu kutokea ajali ya IT na Lori la Mafuta eneo la Iyovi Mikumi Barabara ya Morogoro - Iringa na kuuwa watu watano wakiwemo wanandoa wawili.
Chanzo: EATV