Breaking

Friday, 16 December 2022

BALOZI WA TANZANIA NCHINI AUSTRIA AFARIKI KWA AJALI GARI "MWILI WAKE UMETEKETEA KWA MOTO"


Balozi wa Tanzania nchini Austria na Mwakilishi wa Kudumu wa Mashirika ya Kimataifa Vienna, Celestine Mushy, amefariki dunia katika ajali ya gari huku mwili wake ukiteketea kwa moto katika eneo la Mkata, mkoani Tanga.

Mushi aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan  kuwa Balozi wa Tanzania nchini Austria January mwaka huu na May 5, 2022 akawasilisha hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Austria, Alexander Van der Bellen.

Rais Samia ameeleza kupokea kwa masikitiko taarifa hizo "Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Balozi Celestine Mushi, Balozi wa Tanzania nchini Austria na Mwakilishi wa Kudumu wa nchi yetu katika Mashirika ya Kimataifa, Vienna. Tumeondokewa na mwanadiplomasia mahiri na mtumishi makini wa umma. Mungu amweke mahali pema. Amina."

RPC wa Tanga Henry Mwaibambe ameongea kwa njia ya simu kuhusu ajali ya Balozi Mushi kabla ya Rais Samia kutuma salamu za rambirambi, Kamanda Mwaibambe alisema walikua kwenye utaratibu wa kupima mabaki ya mwili ili kujua kama kweli ni ya Balozi kutokana na kuungua sana kiasi cha kutotambulika kwa macho.

“Ilikuwa ni ajali ya magari mawili kugongana, gari dogo aina ya Toyota Crown Mtu mmoja alikuwa analiendesha na limeungua hadi majivu, baadhi ya Ndugu zake Balozi walikuja wanahisi kwamba ni Balozi, hilo gari kwenye usajili jina linaonesha ni la huyo Balozi kwahiyo ndio maana wanahisi hivyo, tusubiri uchunguzi wa Wataalamu utafanyika kwa haraka tutajua tu”
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages