Jeshi la Polisi wilayani Babati mkoani Manyara, linamshikilia Elias Hando (30) mkazi wa Kijiji cha Tsaayo, Kata ya Arri wilayani humo kwa tuhuma za kumbaka mwanae wa kumzaa mwenye umri wa miaka 6.
Awali mtoto huyo alifanyiwa ukatili wa kubakwa na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Ami Matle, ambaye alifungwa jela miaka 30 ambapo safari hii tena Baba yake mzazi amekamatwa kwa tuhuma za kumbaka mwanae.
Polisi wamemshikilia wanaendelea na uchunguzi wao wakimaliza watamfikisha mahakamani.
Via: EATV