Breaking

Thursday, 15 December 2022

AJIFUNGUA WATOTO TISA KWA MPIGO, WAKIKE WATANO WAKIUME WANNE


Tarehe 4 Mei 2021, itakuwa katika mioyo ya wanandoa wa Mali ambao ulimwengu wao ulibadilika baada ya kujifungua watoto wao tisa mara moja.

Watoto wa Halima Cissé na Kader Arby ni wasichana watano na wavulana wanne.

Wakati Halima Cissé na mumewe Kader Arby mwabaharia katika Jeshi la Wanamaji la Mali walipopata ujauzito hawakutarajia kwamba watapata umaarufu na kuangaziwa kote ulimwenguni. Bila shaka ilikuwa ni ajabu kubwa kwao kuifungua.


Bila shaka ilikuwa ni ajabu kubwa kwao kuifungua watoto tisa kwa mpigi kupitia njia ya upasuaji na wote wakawa na afya nzuri.

Ilikuwa ni jambo la kustaajabisha na pale madaktari wa Mali waliposhindwa kustahimili joto hilo waliona ni bora kumtuma mama mjamzito Morocco.

Wakati alipokuwa akisafirishwa kwa ndege nje kwa mara ya kwanza Halima na familia yake walikuwa wameingiza baridi kuhusiana na hali yake na wanawe.

Madaktari kutoka Mali walihakikisha wanamuweka mama huyo katika hali nzuri ya kiafya kabla ya kumsafirisha hadi Morocco ili aweze kujifungua wanawe kwa njia ya usalama.

Madaktari waliamini watoto hao walikuwa saba ila waliwashtuka walipotokea habari kwamba walikuwa tisa siku ya upasuaji.

Baada ya kujifungua mama na wanawe tisa walipewa makazi ya muda wapone kabla ya kurejea nyumbani hatimaye.

Walikaa katika nyumba ya wauguzi huko Morocco ili waweze kufuatiliwa vizuri na kuangaliwa na madaktari.

Arby, baba yao alikuwa akija na kutembelea mara kwa mara kwani ilimbidi pia kumtunza binti yao wa kwanza Soda, ambaye alibaki nyumbani Timbuktu wakati Cissé alisafirishwa nje.

Mama wa watoto kumi hakufikiria hivyo ndivyo maisha yake yatakavyokuwa.

Serikali ya Mali ilituma wajumbe kukaribisha na kuipokea familia hiyo kwani itachukua watu tisa kuwasaidia wakati na baada ya safari ya ndege hadi watakapofika nyumbani salama.

Kwenye simu Jumapili, Desemba 11, 2022, wanandoa hao waliiambia UK Daily News. Tuna furaha sana hatimaye kuweza kurejea Mali pamoja.

Baada ya kupokelewa na wajumbe nchini humo, watoto hao tisa walipewa cheti kutoka Guinness Book of Records.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages