Watu watatu wamepoteza maisha na wengine 18 kujeruhiwa kwenye ajali iliyohusisha magari manne katika eneo la Nyakato Sokoni jijini Mwanza.
Chanzo cha ajali hiyo kinatajwa kuwa ni gari aina ya TATA lililokuwa limebeba matofali kufeli breki
Ajali hiyo imetokea leo Desemba 1/2022 saa mbili asubuhi ambapo inadaiwa loli hilo lilifeli breki na lilipofika kwenye taa za kuongozea magari katika eneo la Nyakato sokoni ndipo likagonga magari manne na kusababisha ajali hiyo iliyouwa watu watatu huku dereva akikimbia
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Via: EATV