James Kifo Muriuki, mwanamume aliyemshambulia mkewe amehukumiwa kifungo cha miaka 50 jela na Mahakama ya Chuka Law nchini Kenya.
Akiwa mbele ya Hakimu Mfawidhi, Njoki Kahara, mtuhumiwa huyo alipatikana na hatia ya kumlawiti mkewe na kumsababishia madhara makubwa.
James Kifo Muriuki aligonga vichwa vya habari nchini humo baada ya kumdhuru mkewe mnamo Mei 16, 2020.
Inadaiwa wiku ya tukio, Mwanaume huyo alimvuta mkewe hadi mto Kathita huko Marimanti usiku, na kumwamuru avue nguo na kusema/kutaja Wanaume wote aliolala nao alipokuwa akiishi Nairobi.
Ndipo inadaiwa mwanaume huyo alianza kumpiga kabla ya kunyunyizia pilipili, chumvi na gundi (Super Glue) kwenye sehemu zake za siri. Kisha alitumia kisu kusukuma mchanganyiko huo kwenye sehemu ya siri ya mwathiriwa.
Mnamo Mei 21, 2020, Mwanaume huyo alikamatwa katika maficho yake huko Kaningo katika Kaunti ya Kitui na timu ya maafisa wa DCI kutoka kitengo cha Uhalifu Maalum, DCI Tseikuru na DCI kutoka Kaunti Ndogo ya Tharaka Kusini.
Mwanaume huyo alikuwa amejificha kwenye nyumba ya James Murogi ambaye aliaminika kufanya shughuli za uganga, kesi hiyo imekuwa ikiendelea tangu wakati huo huku James akikana kutenda kosa hilo.

Via: Citizen Digital