Breaking

Saturday, 31 December 2022

AFARIKI KWA KUSOMBWA NA MAJI AKIVUKA MTO, WENGINE WANUSURIKA



Benjamin John mkazi wa kata ya Kasamwa halmashauri ya mji Geita, amefariki dunia huku wengine wakinusurika kifo baada ya kusombwa na Maji wakati wakijaribu kuvuka katika mto Nyampa kuelekea kijiji cha jirani.

Baadhi ya mashuhuda wanaeleza kuwa mtu huyo alisombwa na maji akijaribu kuvuka huku wakiiomba serikali kuwajengea daraja kwani eneo hilo limekuwa likichukua uhai wa watu kipindi cha mvua

"Yule mvukaji mwingine alipita lakini yule mwingine wakati anajaribu kupita akawa amezidiwa na maji, basi mwenzake akashindwa jinsi ya kumuokoa akaona kwamba na yeye anaweza kuvutwa kwa sababu mto ulikuwa umefurika maji", alisema Juma moja ya mashuhuda wa tukio hilo

"Hizi ajali za watu kuzama kwenye mto zinatokea mara kwa mara, ningeomba serikali iangakie utaratibu, ikiwezekana watutengenezee madaraja sehemu ambayo watu wanavuka wengi ili kuepusha sanasana hizi ajali na pia huu mto, huwa wanapita mara kwa mara huwa unabeba vitu vingi Sana ikiwemo wakulima hivyo unaharibu mpunga wao", alisema Aloyce.

"Kwamgu mimi nilikuwa naomba serikali itusaidie kuweka daraja inapotokea swala la mto unapita watu wawe wanavuka wanaenda kwenye kazi zao za mashambani", alisema Kabeho.

Mwenyekiti wa mtaa wa Nyampa Helena Maneno anasema katika eneo hilo wameshafariki watu nane kwa kusombwa na maji nyakati tofauti tofauti.

"Mto huu tuseme miaka miwili huwa haipiti bila kuuwa, mara kwa mara huu mto unakuwa unauwa watu, kuna kipindi watoto watatu walifia ndani ya mto huu, kuna kipindi tena kijana mmoja akawa amefia kwenye mto huu ni kama watu wanane wanafika, kwakweli huu mto ni tishio", alisema Maneno

.
Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoa wa Geita limefanikiwa kupata mwili wa marehemu huku mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Kasamwa akikiri kupokea mwili wa marehemu.

"Kwamba kipindi hiki ni mvua za masika na mito inajaa, kwahiyo tuchukue tahadhari, usalama wetu kwanza najua watu wanafanya shughuli za uchumi, kilimo baada ya hapo wanakuwa wamechafuka na kwenda kuoga kwenye mto kwahiyo niwashauri bora waende na ndoo achote maji anawe pembeni au akaoge nyumbani na asijaribu kuyapima maji kwa mguu maji yana pressure Kalu yanaweza yakakupelekea kupoteza maisha", alisema Lukuba.

"Tumempokea wakampeleka Mechwarrior, baada ya kupelekwa Mechwari kufanyiwa uchunguzi wa haraka yani uchunguzi wa awali ambao uliinvolve kumwangalia marehemu kuaniza juu mpaka chini sehemu zote za mwili wake na hatukukuta jeraha licha ya michubuko, obvious ilikuwa ni miba ambao alipokuwa amezama kwenye maji", alisema Alex.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages