Breaking

Wednesday, 23 November 2022

WATU 19 WAKAMATWA TUHUMA ZA WIZI



Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, linawashikilia jumla ya watuhumiwa 19 wanaohusishwa na tuhuma za makosa mbalimbali ikiwemo kupatikana na nyara za serikali (meno ya tembo), nyama ya tandala, dawa za kulevya, mali za wizi pamoja na kupatikana na silaha kinyume cha sheria.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Akizungumza na waandishi wa habari Novemba 23, 2022 katika wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, Kamanda wa Polisi mkoani humo (ACP) Benjamin Kuzaga, alisema kuwa, watuhumiwa wote wamekamatwa kutokana na misako iliyofanyika kuanzia Novemba 11,2022 hadi Novemba 22, 2022 kafka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mbeya.



Aidha, Kamanda Kuzaga, ameendelea kuwataka wananchi na wakazi wa Mkoa wa Mbeya, kuacha kuihujumu serikali kwa kuiba au kuharibu miradi/miundombinu inayojengwa kafika maeneo mbalimbali mkoani humo na kueleza kuwa, Jeshi la Polisi halitamvumilia wala kumuacha mtu yeyote atakayekamatwa kwa tuhuma za uhujumu uchumi au uhalifu wa aina nyingine.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages