Breaking

Wednesday, 9 November 2022

WATOTO WAWILI WAFARIKI, WATATU WAJEHIWA AJALI YA GARI MBEYA



Watoto wawili wamefariki huku Watu watatu wakijeruhiwa kufuatia ajali ya gari iliyotokea eneo la Mlima Iwambi nje kidogo ya Jiji la Mbeya katika Barabara kuu ya Mbeya kwenda Tunduma baada ya Basi kuligonga gari aina ya Toyota Raum.

watoto hao ni wa familia moja ambao ni wanafunzi wa kidato cha pili ambao ni Maria Aluta na Halima Mwaijumba mmoja Shule ya Sekondari St Francis na mwingine Sekondari ya Pandahill.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya Benjamin Kuzaga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo kuwa leo Nov 09,2022 saa 12:45 asubuhi katika eneo la Mlima Iwambi nje kidogo ya Jiji la Mbeya katika barabara kuu ya Mbeya kwenda Tunduma.

Amesema kuwa Basi namba T.601 DXC aina ya Fuso linalofanya safari zake kati ya Mbeya, Tunduma hadi Sumbawanga likitokea Mbeya liligonga gari namba T.452 DHD Toyota Raum na kusababisha vifo vya Watoto wawili waliokuwa kwenye Gari aina ya Toyota Raum.

“Aidha gari hilo T.601 DXC Fuso Bus liliendelea kugonga gari jingine lenye namba za usajili T.673 DMV lenye Tela namba T.362 DMG aina ya Scania lililokuwa linaelekea Mbeya na gari namba DAD 3981 na Tela lake ABF 75591 aina ya Dofeng”

RPC Kuzaga ameeleza kuwa Chanzo cha ajali ni mwendo kasi katika eneo lenye mteremko mkali, jitihada za kumtafuta Dereva zinaendelea, majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu Hospitali ya Rufaa Mbeya.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages