Breaking

Friday, 18 November 2022

WAKAZI KIMARA KUPATA NAFUU HUDUMA YA MAJI KUPITIA VISIMA




Kazi ya kusafisha kisima cha maji cha Kimara baruti kilichopo kata ya Ubungo wilaya ya Ubungo ili kuboresha huduma katika eneo hilo imekamilika.

Kazi hii imehusisha pia upimaji wa ubora wa maji, hii ikiwa ni sehemu ya maandalizi kabla ya kuingiza kisima hicho kwenye mfumo kuhudumia wananchi.

Kisima hiki kina urefu wa mita 60 na uwezo wa kuzalisha lita 48,000 za maji kwa siku.

Kisima kitakapoingizwa kwenye mfumo wa DAWASA wa kuhudumia wananchi na kiatoa huduma kwa kaya takribani 1,900 za Kimara Baruti.

Sambamba na hilo, kazi ya kuboresha kisima cha maji cha Amani kabla ya kukiingiza kwenye mfumo chenye urefu wa mita 86 na uwezo wa kuzalisha lita 35,000 kwa saa imefanyika kikamilifu.

Mpaka sasa DAWASA imefanya maboresho kwenye visima 20 na kufanya jumla ya visima vya DAWASA kuwa 162 vinavyozalisha jumla ya lita 32,037,000 za maji kwa siku.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages