Breaking

Sunday, 6 November 2022

WAKANDARASI KAHAMA WAONYWA KUFANYA UBADHILIFU UJENZI MIRADI YA MAJI



Na Paul Kayanda, Kahama

MKUU wa Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga Festo Kiswaga amesema kuwa fedha alizotoa Rais Samia Suluhu Hassan kwaajili ya miradi ya maji Wilayani Kwake ni zamoto na kuwatahadharisha wakandarasi walioshinda zabuni ya kutengeneza miundombinu hiyo kwamba usitokee ubadhilifu kuhusu fedha hiyo.
Amesema kuwa Rais Samia ametoa fedha kwaajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maji kwenye wilaya yake huku akiwataka wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini RUWASA kuhakikisha wanasimamia miradi hiyo ili ikamilike kwa wakati na kuweza kutoa huduma yamaji safi na salama kwa wananchi.


"Ruwasa hakikisheni wananchi wanapata maji safi na salama, nashukuru kuna maeneo wananchi wanafurahia huduma hiyo muhimu na nawatahadharisha wakandarasi ambao serikali imewaamini mmekabidhiwa dhamana na fedha ili kutekeleza miradi ole wenu miradi isikamilike kwa wakati na hata nyie watendaji wa RUWASA simamieni miradi hiyo kwa uangalifu," alisema DC Kiswaga.





Mhandisi Julieth Payovela ni meneja Ruwasa Mkoa wa Shinyanga amemhakikishia mkuu huyo wa wilaya kusimamia maagizo hayo na fedha zilizoletwa na serikali pamoja na kukamilika miradi hiyo kwa wakati.
"Kwa upande wetu kama RUWASA tuhahika miradi hii inakamilika na hata ifikapo Desemba mwaka huu baadhi ya miradi itakuwa imekamilika na wananchi kuanza kupata huduma ya maji safi na salama," amesema Injinia Payovela.


Ameongeza kuwa kwa mwaka huu wa fedha 2022/2023 serikali imepanga kutumia bilioni 9.8 kwaajili ya kutekeleza miradi yam aji maeneo ya vijijini katika Mkoa wa Shinyanga na kuongeza kuwa mpaka sasa kuna miradi 19 inaendelea kutekelezwa na kughalimi kiasi cha shilingi milioni 35 na kuhakikisha kuwa mpaka Desemba mwaka huu kuna baadhi ya miradi itakuwa imekamilika.

Nao baadhi ya wadau wa mkutano mkuu wa nusu mwaka wa Wilaya ya Kahama wamezungumzia namna wanavyopata adha ya maji huko vijijini na madhara wanayokumbana nayo kwa kuchangia maji na mifugo kama ng’ombe na wanyama wengine kutokana na ukosefu wa huduma hiyo.

Lengo la mkutano mkuu huo lilikuwa ni wadau kujadili, kutathimini,kuelewa na kubadilishana uzoefu kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu maji na usafi wa mazingira.

Mwisho.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages