Na John Mapepele.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa amewatakia kila la kheri wachezaji 10 wa Timu ya Taifa ya Soka kwa Walemavu ( Tembo Warriors) walio sajiliwa na vilabu 5 vinavyo shiriki ligi kuu nchini Uturuki (Amputee football).
Mhe. Mchengerwa ameyasema haya leo Novemba 2, 2022 ambapo amefafanua kuwa tayari wamesafiri leo kwenda nchini Uturuki kwa ajili ya kuanza msimu wa ligi ya Uturuki inayotarajia kuanza Novemba 5, 2022.
Amesema haya ni mafanikio makubwa kwa wacheza na taifa kwa ujumla kwa kuwa dhana na Michezo ni ajira inakamilika.
Ameongeza kuwa dhamira ya Serikali ni kuibua vipaji vya vijana wachezaji wa kitanzania na kuviendeleza ili kuwapa ajira ya uhakika.
Amesema mafanikio haya yametokana na maono na maelekezo mahususi ya Rais Samia Suluhu Hassan katika Michezo.
"Hapa sina budi kumshukuru Mhe. Rais kwa uwekezaji mkubwa alioufanya ambao umezaa matunda na mafanikio makubwa ambayo hayajawahi kutokea katika historia ya nchi yetu". Amesisitiza Mhe Mchengerwa
Vilabu vilivyo sajili wachezaji tembo warriors ni pamoja na klabu ya Sisli Yeditepe ambayo imewasajili Alfan Kyanga, Juma kidevu, Habibu Likoike na Shedrack Hebron.
Klabu ya Keysari imemsajili Abdulkarim Amiri na Salimu Bakari huku klabu ya Konya ikimsajili Ramadhan Chomelo.
Vilabu vingine ni Izmir BBSK iliyomsajili Frank Ngailo huku Klabu ya Mersin ikimsaji Mudrick Azzan na Richard Swai.