Breaking

Friday, 25 November 2022

SERIKALI YAOMBWA KUTOA UFADHILI VYUO VYA KATI



Na Lucas Raphael,Tabora

Chuo Cha Afya Cha Mtakatifu Maximilliancolbe cha mkoani Tabora wameiomba Serikali kuwapatia ufadhili wa masomo kwa vyuo vya kati nchini ili wanavyuo wengi waweze kusoma kama ilivyo vyuo vikuu nchini.

Mkurungezi wa chuo hicho Elizabeth Nkonyoka alitoa kauli hiyo jana katika Mahafali ya Pili ya chuo cha St. Maximilliancolbe yaliyofanyika kwenye viwanja vya chuo hicho Mkoani Tabora .

Alisema kwamba kutokana na mahitaji ya wanafunzi kusoma katika fani mbalimbali wanashindwa kutokana na kukosa ada ,hivyo kuiomba serikali kuwapatia ufadhili kwa vyuo vya kati nchini.

Elizabeth alisema kuwa wengi wa wanafunzi wanaojiunga na vyuo hivyo hawana uwezo kuendelea na masomo kutokana na ada ya masomo kuwa kubwa na hivyo kukatisha ndoto zao za kupata elimu bora.

“wanaiomba Serikali ya awamu ya sita iweze kuwasaidia watoto wanaotoka katika mazingira duni na kuwasaidia kuona jinsi ya kuwasaidia kupata mikopo kwenye vyuo vya elimu ya Kati”alisema Elizabeth Nkonyoka

Mkurungezi huyo wa chuo hicho alisema kwamba kutokana na ufadhili huu ,wahitaji wa misaada ni wengi sana na gharama za uendeshaji kuwa ni kubwa sana na changamoto hiyo inapelekea watoto wengi kuahirisha masomo au kuacha kabisa masomo na kusababisha kukatisha ndoto zao.

Elizabeth alisema kwamba Chuo hicho kimefanikiwa kuwadhamini wanafunzi 25 wenye uwezo mzuri darasani , ambao wanatoka katika familia duni na walioshindwa kumudu kulipa gharama za masomo chuoni hapa kwa kuwalipia gharama zote.

Awali mgeni rasmi kutoka hospitali kuu ya jeshi mkoani Tabora Dkt Luten Kanal Dkt Mikidadi Magogo aliupongeza uongozi wa chuo hicho kwa kutoa elimu bure kwa wanafunzi 25 ambao wataweza kupatikana Madaktari wazuri wenye elimu ya kutosha.

Aliwataka wanafunzi wanaomaliza chuo huko waendako wakafanye kazi kwa weledi na kuwaonea huruma wagonjwa wanaofikishwa katika vituo vyao vya kazi.

Aidha aliwaasa wahitimu hao kuwa na tabia nzuri huko waendako na sio kuharibu cheti chao kwa kupewa sifa mbaya.

Alisema ajira ni wao wenyewe watakapoamua kuchakalika na sio lazima kusubilia ajira za Serikali Kuna taasisi nyingi zinahitaji watabibu na wafamasi kama wao .



Mwisho.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages