Breaking

Wednesday, 2 November 2022

SERIKALI HAITAPUNGUZA ENEO LA HIFADHI YA MSITU WA MBIWE KWA WANANCHI




Serikali imesema haitapunguza eneo la Hifadhi ya Msitu wa Mbiwe kwa ajili ya matumizi ya wananchi na shughuli za kiuchumi ikieleza kuwa itaendelea kulihifadhi eneo hilo kwa lengo la kulinda bioanuai zilizopo katika msitu huo.

Hayo yamesemwa leo Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) , alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Lupa, Mhe. Masache Njelu aliyetaka kujua endapo Serikali inaona haja ya kupunguza eneo la hifadhi ya msitu huo kwa wananchi.

Ameeleza kuwa lengo la kuanzishwa kwa hifadhi hiyo iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya, ni kulinda vyanzo vya maji vinavyotumika kwa matumizi ya binadamu na wanyamapori.

Aidha, amesema Sheria ya msitu huo inaruhusu shughuli za uchimbaji wa madini ndani ya hifadhi kwa kuzingatia kanuni na taratibu zilizopo.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages