Breaking

Saturday, 26 November 2022

MTOTO ASHAMBULIWA NA CHATU AKIOGELEA BWAWANI



Mvulana mwenye umri wa miaka mitano raia wa Australia amenusurika kifo baada ya kuumwa na chatu ambaye ppia alimburuta hadi kwenye bwawa la kuogelea.

Chatu huyo alikuwa na ukubwa wa takriban mara tatu ya umbo la kijana huyo.

Kwa mujibu wa baba yake mzazi Kijana Beau Blake alikuwa akifurahia kuogelea nyumbani kwao wakati chatu huyo mwenye urefu wa mita 3 sawa na futi 10 alipomvamia.

Lakini Beau yuko katika hali nzuri na kwamba anaendelea vyema ingawa ana majeraha madogo tu.

Tukio hilo limeendelea kuzungumziwa katika eneo analoishi kijana huyo.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages